Habari za michezo

SENZO AFUNGUKA MAPYA KUHUSU USAJILI WA MORRISON YANGA NA KUONDOKOKA KWAKE…”UONGO HUPEWA SANA NAFASI TZ”…

admin July 31, 2022 3:40 pm


Saa chache baada ya uongozi wa Yanga kutangaza kwamba aliyekuwa Ofisa Mtendaji wao Mkuu Senzo Mazingiza anaondoka mwenyewe ameibuka na kukanusha juu ya kuondoka kwake kuhusishwa na ujio wa mshambuliaji Bernard Morrison.

Akizungumzia ishu ya kupishana mara mbili na kiungo mshambuliaji Bernard Morrison Senzo amesema wala hana tatizo na usajili huo na kwamba alihusika mara zote kumsajili Mghana huyo katika klabu zote.

“Niliwahi kuwaambia  juu ya Morrison, bahati mbaya hapa Tanzania uongo hupewa nafasi kubwa kusambaa, nilisema nilipokuwa Simba nilihusika kumleta Morrison pale lakini bahati mbaya wakati anafika mimi nilikuwa naondoka,” amesema Senzo

“Nikiwa hapa Yanga pia imekuwa hivyohivyo, viongozi wenzangu wanajua jinsi tulivyoshirikiana kumleta huyu Morrison, huyu ni mchezaji bora bila kuangalia mambo yake yanayosemwa.

“Nina imani kubwa Morrison atakwenda kuwafanyia kazi kubwa wananchi ambao wamempokea tena bila kinyongo, hata mimi nitafarijika nikisikia Morrison akiwa anafanya kazi bora hapa.

“Mimi bado ni mwananchi hapa nitaendelea kuwasailiana na viongozi wenzangu, sijaondoka Yanga kwa ubaya kabisa ndio maana mmekuwa mkiniona hapa katika kazi zote, bahati mabya hili lilitakiwa niliamue sasa wakati ambao pia mkataba ulikuwa unakwisha.

SIKU KADHAA BAADA YA YANGA KUZINDUA JEZI…SIMBA WAIBUKA NA KUTAMBA KUHUSU JEZI ZAO..WADAI ZINATOKA ULAYA… SAKHO AVUNJA UKIMYA SIMBA…AFUNGUKA ALICHOAMBIWA NA SADIO MANE…AANIKA TIMU ZILIZOMFUATA KUMTAKA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply