Home Habari za michezo A-Z JINSI BANGALA ALIVYOWAKA TUZO ZA TFF JANA…AMGARAGAZA INONGA WA SIMBA…WASHINDI WENGINE...

A-Z JINSI BANGALA ALIVYOWAKA TUZO ZA TFF JANA…AMGARAGAZA INONGA WA SIMBA…WASHINDI WENGINE HAWA HAPA…


Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/22 imeenda kwa kiungo wa Yanga ambaye ni raia wa Congo DR, Yaniki Litombo Bangala.

Tuzo hizo zimetolewa leo na TFF katika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam ambapo Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo Senzo Mbatha Mazingiza amepokea tuzo hiyo kwa niaba ya Bangala.

Bangala ameisaidia Timu yake ya Yanga kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC bila kusshindwa na kutwaa Kombe la Shirikisho bila kushindwa.

Bangala anatajwa kuwa mwiba kwa wapinzani wakati timu yake ikicheza. Anatajwa kuwa mmoja wa viuongo wazuri kwenye kupora mipira, kuanzisha mashambulizi na kupiga pasi zenye ufasaha.

Aidha, mchezaji huyo ana sifa nyingine ya kucheza nafasi nyingi zaidi uwanjani kutokana na majukumu anayopewa na mwalimu wake.

Kocha Nasreddine Nabi wa Yanga amekuwa akimtumia Bangala kama kiuong na wakati mwingine kama beki wa kati lakini Mkongomani huyo amekuwa akimudu nafasi zote na kucheza vizuri.

Tuzo ya mchezaji bora wa ASFC ilikuwa kiwaniwa na Sopu wa Coastal Union, Feisal na Fiston Mayele wote wa Yanga wakati tuzo ya mchezaji bora wa SWPL ikiwaniwa na Asha Djafar wa Simba Queens, Amina Millal wa Yanga Prencesss na Fatma Issa wa Simba Queens.

Mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara iliwaniwa na Inonga wa Simba, Bangala na Mayele wote wa Yanga wakati mchezaji bora wa Championship ikiwaniwa na Edward Songo wa JKT Ruvu, Kenani Mwelukilwa wa Kitayosce na Mohamed Haji wa Mashujaa.

Tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Daraja la Kwanza iliwaniwa na Selemani Kibuta wa Alliance, Mohamed Hussein wa Capco Veteran na Yassin Mgaza wa Mbuni.

TUZO ZA MCHEZAJI BORA WA MSIMU(MVP) 2021/22.

Mchezaji bora SWPL Fatma Maonyo (Simba queens)

Mchezaji bora FA CUP Abdul Suleman (Coastal Union)

Mchezaji bora NBC PL Yanick Bangala (Yanga SC)

Edward Songo wa JKT – mchezaji bora wa ligi daraja la kwanza (Championship).

SOMA NA HII  MASTAA HAWA WA YANGA 'WAMTIA TUMBO JOTO' KOCHA WA CR BELOUIZDAD...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here