Home Habari za michezo BANGALA ARUDI YANGA NA MZUKA KAMA WOTEE…AKUTANISHWA NA GSM WAKUBALIANA MAMBO HAYA...

BANGALA ARUDI YANGA NA MZUKA KAMA WOTEE…AKUTANISHWA NA GSM WAKUBALIANA MAMBO HAYA MAPYA…


Kikosi cha Yanga juzi asubuhi kilifanya mazoezi viwanja vya Gymkhana na jioni kikarudi Avic kwa mechi ya kirafiki ya kujipima nguvu, huku kiungo fundi wa timu hiyo, Yannick Bangala akitua na mkwara kambini kwa ajili ya kuanza maandalizi ya msimu mpya wa mashindano.

Bangala alichelewa kuungana na wenzake kutokana na ruhusa maalumu baada ya kumaliza likizo yake na juzi alirejea na moja kwa moja kwenda kuonana na uongozi wa klabu hiyo kwa ajili ya kujadiliana juu ya maslahi na dili la kuongezewa mkataba mpya.

Kiungo huyo aliyetwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu uliopita akiwa pia ndiye Kiungo Bora wa Ligi Kuu alitua Yanga msimu uliopita kutoka Far Rabat ya Morocco kwa mkataba wa miaka miwili na ameshatumikia mwaka mmoja hadi sasa, huku ikielezwa alikuwa akitaka kuboreshewa maslahi kabla ya kusaini mkataba mpya.

“Jamaa kesharudi na jana (juzi) alikutana na viongozi ili kujadilia ishu zake za mkataba mpya, lakini hawakupata muafaka na sasa anamsikilizia GSM, ili kuweka mambo sawa, ila amesisitiza msimu huu amekuja kivingine akiwa na kiu ya kutaka kuona Yanga inafika mbali zaidi,” chanzo makini kutoka kwa mtu wa karibu wa Bangala .

“Nadhani kila kitu kitaenda sawa kama ilivyokuwa kwa Fiston Mayele ambaye anatarajiwa kusaini mkataba mpya Agosti, ingawa wamekubaliana na kigogo (GSM) kila kitu ikiwamo kuongezewa mshahara kutoka ule wa awali (kiwango tumekihifadhi),” kiliongeza chanzo hicho.

Kutua kwa Bangala kunaifanya kazi ya Yanga kukamilika na kumrahisishia kazi kocha Nasreddine Nabi na wasaidizi wake kuiandaa timu kwa msimu ujao, ikijiandaa pia na mechi ya kilele cha Wiki ya Mwanachi itakayofanyika Agosti 6 kabla ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba itakayopigwa Agosti 13.

Yanga inatarajiwa kuwa wenyeji wa Red Arrows ya Zambia kwenye siku ya kilele cha Wiki ya Wananchi itakayopambwa na burudani mbalimbali.

Msimu uliopita Yanga ilibeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara bila kupoteza mechi ikifikisha jumla ya michezo 37 iliyocheza ikiisaka rekodi ya Azam ya kucheza mechi 38 mfululizo bila kupoteza, lakini ikitwaa pia Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na Ngao ya Jamii – mataji yote yalikuwa yakishikiliwa na Simba.

SOMA NA HII  MAYELE LIMEMKUTA JAMBO YANGA..NABI AMPA ONYO...PABLO AITISHA KIKAO..MATOLA ATOA KAULI YA KIBABE...