Home Habari za michezo DODOMA JIJI NAO WAAMUA KUFANYA KWELI…WAMVUTA BANGALA NDANI YA NYUMBA..SASA NI ‘UNDAVA...

DODOMA JIJI NAO WAAMUA KUFANYA KWELI…WAMVUTA BANGALA NDANI YA NYUMBA..SASA NI ‘UNDAVA UNDAVA’ TU…


Dodoma Jiji ni mwendo wa kutoa wachezaji nje ya nchi, baada ya Ghana sasa ni zamu ya DRC Congo.

Uongozi wa klabu hiyo umemtambulisha rasmi mshambuliaji Randy Bangala ambaye ni mdogo wake na kiungo wa Yanga Yannick Bangala kuitumikia timu hiyo msimu huu wa Ligi Kuu ya NBC.

Tayari Klabu hiyo imeshawatangaza wachezaji wawili raia wa Ghana ambao msimu uliopita waliichezea Biashara United.

Klabu hiyo ilimtambulisha kiungo ambaye hucheza dimba la chini ama la juu  Christain Zigar na jana ilimtambulisha  Collins Opare ambaye hucheza Striker.

Randy  hucheza nafasi ya ushambuliaji mara ya mwisho aliichezea timu ya TP Les Croyant ya DRC Congo  na  amewahi kuzichezea  timu za Fc Renaissance,Jeunesse Sporting Tsangu na  AS Maniema Union za DRC Congo.

Striker huyo anaenda kuimarisha sehemu ya ushambuliaji  ya timu hiyo kufuatia Anuary Jabir kujiunga na Kagera Sugar.

Miongoni mwa majina ambayo yanatajwa kusajiliwa na timu hiyo na wanaosubiri kutangazwa ni Jimmy Shoji kutoka Mbeya Kwanza, Amaan Kyata kutoka Coastal Union, Hassan Mwaterema kutoka Kagera Sugar  na wengineo ambao majina yao wamefichwa.

SOMA NA HII  PAMOJA NA 'SONGOMBINGO' ZA TFF NA BODI YA LIGI KWAKO...SIMBA WAMWAGA 'KONGELO' ZA 'KUFA MTU' ...