Home Habari za michezo NI YANGA TENA….WABEBA TAJI LA KOMBE LA SHIRIKISHO KWA MBINDEEE…COASTAL UNIONI WAKIFA...

NI YANGA TENA….WABEBA TAJI LA KOMBE LA SHIRIKISHO KWA MBINDEEE…COASTAL UNIONI WAKIFA KIUME…


Hawakamatiki. Ndicho unachoweza kusema baada ya jioni ya leo Timu ya Yanga ambao pia ndio mabingwa wa Ligi Kuu Bara 2021/2022 kufanikiwa kunyakua kombe la Azam Sports Federation Jijini Arusha.

Fainali hiyo iliyokuwa ya piga nikupige iliamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya Penati baada ya sare ya magoli 3-3 katika dakika 120.

Yanga walitupia nyavuni penati 4 zilizopigwa na Bangala, Job, Makambo na Aucho huku Coast wakifunga penati 1 na kukosa mbili.

Mbali na Yanga kubeba ubingwa habari kubwa ni kiungo mshambuliaji wa Coastal Union Abdul suleiman Sopu alietupia magoli matatu kwenye mchezo wa leo.

Magoli ya Yanga yalifungwa na Feisal, Makambo na Denis Nkane dakika za lala salama, alieingia kuchukua nafasi ya Bakari Mwamnyeto.

SOMA NA HII  WAAMUZI WA TANZANIA,PEPERUSHENI BENDERA KIMATAIFA