Home Geita Gold FC PAMOJA NA KUFANYA KAZI NZURI MSIMU HUU…GEITA GOLD WAMTEGA ‘KININJA’ MINZIRO…AAMBIWA NI...

PAMOJA NA KUFANYA KAZI NZURI MSIMU HUU…GEITA GOLD WAMTEGA ‘KININJA’ MINZIRO…AAMBIWA NI JUU YAKE KUJIMALIZA…


Hatma ya Kocha wa Geita Gold, Fred Felix ‘Minziro’ iko mikononi mwake endapo ataona mkataba mpya unamfaa kuendelea kuinoa timu hiyo kwa msimu ujao.

Minziro baada ya msimu kumalizika kwa mkataba wake ulifika kikomo na sasa viongozi wako katika mipango ya kumuongezea ili aendelee kuliongoza jahazi la timu hiyo.

Akizungumza Mwenyekiti wa timu hiyo, Costantine Molandi alisema jana kuwa viongozi walikutana kwa mara nyingine kupanga mipango ya maandalizi ya msimu.

“Leo (jana) tutakuwa na kikao kingine na ndicho kitakuwa na maazimio ya timu iweke wapi camp (kambi) kwa ajili ya msimu ujao sambamba na masula ya usajili,” alisema Molandi.

Aidha Molandi alisema, ubora aliouonyesha Minziro ndani ya kikosi chao ulisababisha timu kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa imewafanya waendelee kuhitaji huduma yake.

“Tunachokifanya sisi ni kuongea nae na kumuonyesha ofa ya mkataba wetu, sasa akiamua kubaki ni yeye endapo ataona maslahi yanamruhusu, ila sisi tunatamani kuendelea naye,” alisema Molandi.

Minziro alipoulizwa juu ya hatima yake ndani ya kikosi hicho amesema:

“Bado hawajaniita mpaka sasa, tukielewana nitaendelea kuinoa timu.”

SOMA NA HII  JE MASHINE HII YA MAGOLI INAWEZA KUWA TOFAUTI NA WAGHANA WENGINE AKIJA SIMBA?