Home Habari za michezo SAKATA LA KUFUNGIWA NA TFF…MANARA AMSHUKIA WAZIRI WA MICHEZO…”KAMA ULIVYOSEMA NIADHIBIWE…KASIMAMIE KATIBA”..

SAKATA LA KUFUNGIWA NA TFF…MANARA AMSHUKIA WAZIRI WA MICHEZO…”KAMA ULIVYOSEMA NIADHIBIWE…KASIMAMIE KATIBA”..


Msemaji wa Yanga Haji Manara ameongea na waandishi wa habari kuelezea sakata lake la kufungiwa kujihusisha na masuala ya michezo ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miaka 2 pamoja na faini ya shilingi milioni 20.

Manara amemtaka Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa kwenda kusimamia haki ya kiapo chake cha Katiba kwa kuhakikisha kanuni zilizotumika kumfungia zinakuwa ni kanuni halali ambazo zimesajiliwa.

“Kwa minajili hiyo mimi na Mchengerwa wote Wandengereko na naamini wandengereko wote tunasimama na haki, Waziri wangu Mchengerwa kasimamie haki ya kiapo chako cha katiba kwamba huwezi kuruhusu kama ulivyosema siku ile kwa mbwembwe kwamba niadhibiwe basi nenda kwa mbwembwe hizohizo kasimamie utekelezaji wa kwamba kanuni lazima zisajiliwe.” Amesema Manara.

Aidha Manara amesema yeye bado ni msemaji halali wa Yanga kwani hajapewa nakala ya hukumu yake ambayo ndiyo inampatia haki ya kukata rufaa.

Akiongea kuhusu sakata la kumtukana Rais wa TFF Wallace Karia amesisitiza kuwa hajafanya kosa kama hilo na hajamtukana Rais Karia zaidi yeye nduyi aliyekosewa na imekuwa ni muendelezo wa kupewa kauli chafu na za kudhalilishaji kutoka kwa Rais huyo wa TFF.

SOMA NA HII  BAADA YA KUWAGOMEA...GEITA WAAMUA KUMALIZANA MAZIMA NA NTIBAZONKIZA...