Habari za michezo

BAADA YA KULAMBA ‘SHAVU’ YANGA… BOSI WA ZAMANI KMC AIBUKA NA KUANIKA HAYA HADHARANI…AMTAJA KATIBU WA CCM…

admin August 1, 2022 11:01 am


WALTER Harson aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa KMC ameweza kuwashukuru maosi wake hao na sasa anakwenda kuanza changamoto mpya ndani ya kikosi cha Yanga.

Ujumbe wake ambao amewaandikia mashabiki wake pamoja na KMC unasomeka namna hii:”Imekuwa miaka minne yenye kujifunza na kukua katika tasnia. Nafasi niliyoipata ya kuhudumu kama Mtendaji Mkuu wa Klabu kwa kipindi chote cha miaka minne imenifanya kuwa huyu niliye kwa sasa.

“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi wa Manispaa ya Kinondoni, wa zamani wakati nakuja chini ya Mkurugenzi Aron Kagurumjuli, Meya Benjamin Sitta na Mkuu wa Wilaya Daniel Chongolo kwa ushirikiano ulioweza kutupa mafanikio kwa uchanga tuliokuwa nao kwa wakati huo.

“Napenda pia kuushukuru uongozi wa sasa chini ya Mkurugenzi Hanifa Hamza, Meya Songoro Mnyonge na Mkuu wa Wilaya Godwin Gondwe kwa jinsi wanavyoendelea kushirikiana kuhakikisha malengo ya kuifikisha KMC FC juu zaidi.

“Namshukuru Mwenyekiti wangu Kheri Missinga, technical bench, wachezaji na mashabiki kwa nyakati zote tulizokuwa pamoja katika kipindi cha miaka minne.

“Imefika wakati wa kwenda kupata changamoto nyingine hivyo napenda kuwaaga na kuwatakia kila la kheri katika msimu mpya 2022/2023 nikiwa na imani kuwa unaenda kuwa msimu wa mafanikio makubwa kwenu

“Nimejifunza mengi katika kipindi chote na nitakuwa shabiki wa KMC FC daima kwa historia mliyoitengeneza kwenye maisha yangu,” .

M-BET WAIMWAGIA SIMBA BILION 26 ZA UDHAMINI….MKATABA WAO NI WA KIHISTORIA TOKA TANZANIA IUNDWE… MANARA TENA….BAADA YA KUMLIPUKIA WAZIRI MCHENGERWA…LEO AIBUKA NA HILI JIPYA…ADAI ALIINGIA KICHWA KICHWA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply