Kocha wa ZED FC Ammwagia Sifa Kem Kem Florent Ibenge wa Azam FC!
Ibenge amejijengea heshima kubwa kupitia kazi nzuri aliyoifanya katika klabu na timu za taifa, akishiriki mashindano makubwa yaliyompa uzoefu wa kukabiliana na presha ya kimataifa:
-
Timu ya Taifa (DR Congo): Aliiongoza DR Congo kumaliza nafasi ya tatu kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2015 nchini Equatorial Guinea, na kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndania (CHAN) mwaka 2016.
-
AS Vita Club: Aliifikisha timu hiyo katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2014.
-
RS Berkane (Morocco): Aliiongoza kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2022 baada ya kuifunga Orlando Pirates kwa mikwaju ya penalti.
-
Al Hilal (Sudan) & Azam FC (Tanzania): Baada ya kupita Sudan, alijiunga na Azam FC na msimu uliopita aliipa rekodi ya kihistoria ya kufika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Huu ukiwa ni msimu wake wa pili ndani ya Azam FC, Ibenge analenga kufanya makubwa zaidi kwenye Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho la CRDB, pamoja na hatua ya makundi barani Afrika.