Azam FC vs ZED FC
Azam FC

Azam FC Yamlazimisha ZED FC Sare Ugenini Misri – Kombe la Shirikisho

Vardo October 17, 2026 9:29 am

Dar es Salaam. Azam FC imejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya ZED FC ya Misri, kwenye mchezo uliochezwa Ijumaa, Oktoba 16, 2026.

Wenyeji ZED FC ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 45 kupitia kwa Mahmoud Shokry. Shokry alifunga bao hilo kwa shuti kali la mguu wa kulia akimalizia mpira uliotemwa na kipa tegemeo Aishi Manula, kufuatia kona iliyochongwa kwa ustadi na timu hiyo ya Misri. Bao hilo lilidumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi tofauti, huku Wawakilishi hao wa Tanzania bara wakionyesha kiu ya kusawazisha. Juhudi zao zilizaa matunda katika dakika ya 58 kupitia kwa kiungo mshambuliaji mahiri, Iddy Seleman ‘Nado’, aliyetumia vyema pasi ya Pascal Msindo kufunga kwa shuti kali la mguu wa kulia.

Nini Kinafuata Kwenye Mechi ya Marudiano? Matokeo haya yanaiacha Azam FC ikihitaji ushindi wa aina yoyote katika mchezo wa marudiano utakaopigwa mwishoni mwa wiki ijayo nyumbani katika Uwanja wa Azam Complex, ili kutinga rasmi hatua ya makundi.

Pamoja na ushindi, Azam pia inaweza kusonga mbele ikiwa mchezo huo utamalizika kwa sare ya bila kufungana (0-0). Hata hivyo, kama mechi hiyo ikimalizika kwa sare ya bao 1-1, mshindi atapatikana moja kwa moja kupitia mikwaju ya penalti. Mambo yatakuwa magumu iwapo ZED FC ipata ushindi ugenini.

Timu hiyo inasaka kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya pili mfululizo, ambapo msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya tatu kwenye kundi lake baada ya kukusanya pointi tisa.

Kocha wa ZED FC Ammwagia Sifa Kem Kem Florent Ibenge wa Azam FC! Ratiba ya Raundi ya Sita Ligi ya Championship 2026: Vita ya Kileleni na Matokeo Yake