Habari za michezo

PAMOJA NA KUWA MTU MUHIMU SANA SIMBA….MAGORI AJITOSA KWENYE SIASA RASMI…AOMBA UBUNGE WA….

admin August 7, 2022 7:00 am


Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa klabu ya Simba, Crescentius Magori ni mmoja ya waliojitokeza kuomba ridhaa ya CCM kuchaguliwa kugombea ubunge wa Afrika Mashariki.

Magori ambaye pia ni mshauri wa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Simba amechukua fomu hiyo leo ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Agosti  5, 2022 Jijini Dodoma Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Oganaizesheni, Maudline Castico amesema mbali na Magori wanachama wengine 94 wameomba  ridhaa ya kugombea  nafasi hizoo ndani ya chama.

Ongezeko la wanachama hao limezidi kuongeza joto la uchaguzi huo kwani nafasi zinazohitajika ni tisa tu lakini wagombea wamefika 94 na kuna uwezekano wakaongezeka kwani siku ya mwisho kuchukua fomu ni Agosti 10.

KUELEKEA MSIMU MPYA….HENOCK INONGA AFUNGUKA NAMNA WATAKAVYOJENGA UKUTA WA ROMA KWA SIMBA… MFAHAMU STAA MKUBWA WA SOKA DUNIAN ANAYELIPWA BILION 26 LAKINI BADO ANAISHI KWA WAZAZI WAKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply