Habari za michezo

KISA JEZI NPYA SIMBA…MASHABIKI WAMKATAA FRED VUNJA BEI…WALIA BEI KUUZWA ZAIDI YA 150000 …

admin August 8, 2022 4:12 pm


Sakata la jezi mpya za Simba SC limechukua sura mpya leo Agosti 8 kwa muuzaji mkuu wa Jezi hizo mfanyabiashara Fredrick Ngajilo “Fred Vunjabei”.

Baada ya mashabiki kutangaziwa uwepo wa jezi hizo katika maduka ya Vunja bei walifurika kununua jezi hizo mpya za Simba zilizokuwa zikiuzwa kwa kiasi cha Tsh 35000/=.

Lakini Leo mapema kulitoka taarifa kuwa jezi hizo zimekwisha hivyo umati wote uliokusanyika katika duka la Vunja bei walijikuta wakinyong’onyea.

Lakini katika hali isiyo ya kawaida wameibuka watu (vishoka) ambao wanauza jeI kwa bei ya Tsh 150000 mpaka laki 200000 hivyo kuzua minong’ono kwa mashabiki ya kutaka kujua jezi hizo wametoa wapi.

Katika hali ya kushangaza mashabiki hao walianza kuimba wakisema hawamtaka Fred Vunja bei kuwa muuzaji na msambazaji wa jezi za Simba.

Meridianbet Wawatembelea Boda Boda, Wawapa Ujumbe Usalama ni Muhimu #SIMBADAY: SIMBA WALIVYOIGARAGAZA YANGA KWA MKAPA LEO….MBABE WA MANDONGA AIBUA SHANGWE UWANJA MZIMA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply