Habari za michezo

PAMOJA NA KUTOPEWA MKATABA MPYA…SIMBA WAKUBALI KUENDELEA ‘KUISHI’ NA HASSAN DILUNGA KWA STAILI HII…

admin August 8, 2022 11:50 am


Licha ya mkataba wake kumalizika, lakini kiungo wa Simba, Hassan Dilunga ataendelea kulipwa kiasi cha pesa kutoka kwa waajiri wake hao kwani majeraha yanayomuweka nje ya uwanja aliyapata akiwa anaitumikia timu.

Dilunga aliumia kifundo cha mguu wakati wakijiandaa na mechi dhidi ya Orlando Pirates hivyo jeraha hilo lilimfanya afanyiwe upasuaji Afrika Kusini na kushindwa kumalizia mechi za msimu uliopita.

Habari za ndani kabisa kutoka ndani ya Simba zinaeleza mabosi wa klabu hiyo wanaamini Dilunga ni kiungo bora ingawa hayumo kwenye usajili wa msimu huu, lakini watamsikilizia hadi wakati wa dirisha dogo kuona maendeleo yake ndipo watampa mkataba mwingine.

Chanzo kilisema japo mchezaji huyo ameanza mazoezi binafsi, lakini hawezi kucheza mechi za mashindano kwani akifanya hivyo anaweza kupata jeraha kubwa.

“Viongozi wamekubaliana pamoja kuwa Dilunga alitoa mchango mkubwa kwenye timu, hivyo kipindi hiki ambacho atakuwa nje ya uwanja akijiunguza atakuwa analipwa kiasi cha pesa kitakachomsaidia.

“Hayumo kwenye usajili wa msimu huu, lakini anaweza kuongezwa mkataba wakati wa dirisha dogo. Pesa atakayolipwa inaweza kuwa nusu mshahara aliokuwa akiupata ama kiasi watakachoona kinafaa kumpatia,” kilisema.

“Tumeamua kufanya hivi kwa sababu aliumia akiwa kwenye majukumu ya timu, hivyo haitakuwa busara kumuacha hivihivi wakati jeraha kwa mujibu wa daktari litapona kwa kipindi fulani.”

#SIMBADAY: MKUDE AWEKA REKODI YA KIBABE SIMBA…MAKOCHA 14 WAPITA NAYE JUU KWA JUU… YANGA WAIFANYIA UMAFIA SIMBA KWENYE DILI LA MANZOKI…NABI AINGILIA MCHEZO NA KUHARIBU MAMBO USIKU USIKU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

One response to “PAMOJA NA KUTOPEWA MKATABA MPYA…SIMBA WAKUBALI KUENDELEA ‘KUISHI’ NA HASSAN DILUNGA KWA STAILI HII…”

  1. Yohana kisumo Yohana says:

    Soka

Leave a Reply