Habari za michezo

‘VIBE’ LA MASHABIKI WA SIMBA JANA KWENYE SIMBA DAY LAMPAGAWISHA MANZOKI…AKUBALI KILA KITU…

admin August 9, 2022 8:51 am


Mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati Cesar Lobi Manzoki, ameipongeza Simba SC, kwa kufanikisha Tamasha la Simba Day jana Jumapili (Agosti 08), Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Manzoki ambaye anahusishwa na usajili wa Simba SC, ametoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuweka picha ya pamoja ya wachezaji na Benchi la Ufundi iliyopigwa baada ya kutambulishwa katika Tamasha hilo.

Manzoki ameandika: Hongera @simbasctanzania kwa kufanikisha hili, ilikua siku nzuri kwa Mashabiki wa Simba, ninakubali klabu hii ni kubwa Barani Afrika.

Mshambuliaji huyo alikuja Dar es salaam akiwa na kikosi cha Klabu yake ya Vipers SC ya Uganda, kwa ajili ya mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Young Africans katika Kilele cha Wiki Wananchi Jumamosi (Agosti 06).

Mchezo huo ulimalizika kwa Vipers SC kushinda 2-0, huku Manzoki akiwekwa Benchi.

Dili la Manzoki kujiunga na Simba SC linatajwa KUFELI kutokana na Uongozi wa Vipers SC kuhitaji kiasi kikubwa cha pesa ili kuvunjwa kwa mkataba wake uliosaliwa na muda wa miezi miwili.

ALICHOSEMA KAGERE BAADA YA KUSHUKA KWENYE JUKWAA LA SIMBA…AFUNGUKA MENGINE MAPYA USIYOYAJUA… BAADA YA KUIONA SIMBA INAVYOCHEZA JANA ….MCHAMBUZI NGULI AMSHUKIA KOCHA MAKI…AMPA ONYO LA YANGA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply