CAF

HII CAF SUPER LEAGUE NI SUPA KWELI KWELI AISEE…BINGWA KUKOMBA ZAIDI YA BILIONI 200..WAKATI TIMU SHIRIKI ZIKIPEWA BIL 6…

admin August 10, 2022 2:20 pm


Hatimaye Kitendawili cha Michuano ya CAF Super League kimeteguliwa mjini Arusha-Tanzania, kwa Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ Patrice Motsepe kutoa ufafanuzi wa kina.

Rais Motsepe amesema michuano hiyo ambayo itachezwa kwa mara ya kwanza Barani Afrika itashirikisha klabu 24, ambazo zitanufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na Bajeti iliyotengwa na CAF.

Amesema Bingwa wa Michuano hiyo atavuna kasi kikubwa cha pesa Dola milioni 100 za Marekani Zaidi ya Bilioni 200.

Akiwa katika Mkutano Mkuu wa CAF mjini Arusha leo Jumatano (Agosti 10) kiongozi huyo amesema: “Ukiacha viwanja tatizo kubwa kwa mpira wa bara la Afrika ni fedha”

“Nimshukuru kaka yangu Gianni Infantino kwa kutupatia wazo hili ambapo kupitia mashindano haya mapya ya CAF SUPER LEAGUE klabu zitapata fedha nyingi ambapo kwa kuanza kila klabu shiriki itapata dola milioni 2.5  sawa na Bilioni 6 na ushehe kwa ajili ya kusajili wachezaji na gharama za michuano kama usafiri na hotel lakini pia bingwa atapata dola za Marekani Milion 100.”

ISHU YA KUWAONGEZEA MIKATABA MINONO BANGALA NA DJUMA…RAIS YANGA AIBUKA NA KUJIBU HOJA HIZI… BAADA YA KUONA SIMBA NA AZAM WAKO ‘SIRIAZI’ SANA NA UBINGWA…YANGA WASHTUKA…WAUNDA KIKOSI KAZI CHA USHINDI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply