Habari za michezo

BAADA YA MASHABIKI KUANZA KUMNANGA….UONGOZI SIMBA WATOA NENO KWA STRAIKA ‘MZUNGU’…WAMPA MUDA….

admin August 16, 2022 6:58 pm


Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema klabu hiyo imeamua kuachana na dili la kumsajili mshambuliaji nyota wa Vipers United ya Uganfda, Cesar Manzoki kutokana na sintoifahamu katika mkataba wake.

Kauli hiyo ya Ahmed inakuwa ikiwa ni baada ya maneno mengi ya mashabiki wanaodai kuwa Simba kwa sasa hawana mshambuliaji mzuri hata Dejan raia wa Serbia aliyesajiliwa hivi karibuni, hana uwezo ule uliotarajiwa.

“Dejan mpaka amesajiliwa ina maana kamati husika imejiridhisha kwamba atatusaidia, tumpe muda ni kweli kwenye hizi mechi mbili hakufanya vizuri sasa tunaenda kuanza Ligi na Geita tunaamini tutamungalia vizuri.

“Ni kweli nilimtambulisha kama mzungu kwangu mimi sio tatizo, pengine kwa sasa inaonekana kama dhiaka kwa kuwa hajafunga ila kwangu nachukulia ni jambo chanya,” amesema Ahmed Ally.

KIPIGO CHA 4-0 KUTOKA BRIGHTON CHAWAINUA MASHABIKI MAN UTD…WIBUKA NA MSIMAMO HUU MKALI KWA WENYE TIMU… GOLI LA KIBRAZILI LAITAKATISHA SINGIDA BIG STARS MBELE YA TZ PRISONS…AMISI TAMBWE ‘MIBICHWA’ ATIKISA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply