Habari za michezo

FENERBAHCE WAMCHEUA TENA SAMATTA….GENK WAMDAKA TENA JUU KWA JUU….

admin August 16, 2022 2:42 pm


BAADA ya miaka miwili, miezi saba na siku 16 hatimaye Mbwana Samatta amerejea tena KRC Genk, timu ya kwanza kuichezea barani Ulaya na kupata mafanikio makubwa ikiwa pamoja na kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu nchini Ubelgiji.

Samatta amereja Genk kwa mkopo wa msimu mmoja wenye kipengele cha kumnunua mazima akitokea Fenerbahce ambako hakuwa anapata nafasi ya kucheza tangu alipotua akitokea Aston Villa.

Hii itakuwa ni mara yapili Samatta kutolewa kwa mkopo na Fenerbahce baada ya mara ya kwanza kupelekwa Royal Antwerp ya huko nchini Ubelgiji.

Mkataba wa sasa wa staa huyu na Fenerbahce  unatarajiwa kumalizika mwaka 2024.

Mbali ya kuchukua ubingwa akiwa na Genk msimu wa 2018/19, Samatta pia aliibuka kuwa mfungaji bora baada ya kuingia kambani mara 20.

BAADA YA KUSEMEWA MBOVU SANA NA MASHABIKI…’MZUNGUU’ WA SIMBA AJITIA KITANZI CHA AHADI…. FT: POLISI TZ 2-1 YANGA SC….MAYELE ATUPIA KIMYA KIMYA….MWAMNYETO AOKOA CHAMA LA KIJANI….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply