Habari za michezo

BAADA YA KUONA ‘STRAIKA MZUNGU’ WA SIMBA ANAVYOCHEZA….ULIMBOKA MWAKINGWE KAGUNA KISHA AKASEMA HAYA….

admin August 17, 2022 1:02 pm


Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC Ulimboka Mwakingwe amesema Mshambuliaji mpya wa klabu hiyo Dejan Georgijevic ana uwezo mkubwa kisoka, na ana matarajia makubwa ya kuona akiwashangaza wanaombeza.

Mwakingwe ambaye kwa sasa ni Kocha wa Soka, amesema amemfuatilia Dejan tangu alipowasili nchini na kujiridhishwa ana uwezo wa kupambana, ila amecheza michezo miwili iliyokuwa na ushindani mkubwa na uhitaji wa matokeo mazuri.

Amesema Mashabiki wa Soka la Bongo wamekua na shauku ya haraka kuona Mshambuliaji huyo kutoka nchini Serbia anafanya makubwa, lakini kwake anaendelea kumpa muda na anaamini atafanikiwa.

“Nimeona mikimbio yake na aina yake ya kucheza ni moja ya mastraika wanaopenda kuwekewa pasi kwenye njia na kufunga kama itatokea kuna kiungo wa Simba akamjulia katika hilo atafanya vizuri,”

“Unajua Mashabiki wengi wa Tanzania wamekua na kasumba ya kutaka kuona vitu vikitokea kwa haraka haraka, lakini kwangu mimi sipo hivyo, ninaamini huyu jamaa atawashangaza wengi, hapa kinachomsumbua ni mfumo wa timu lakini akishafahamiana vizuri na viungo, hapo mambo yatamnyookea.” amesema Ulimboka.

Dejan amesajiliwa Simba SC baada ya kupendekezwa na Kocha Mkuu Zorana Maki, huku akichukua nafasi ya Washambuliaji Meddie Kagere na Chriss Mugalu ambao waliachwa kwenye usajili wa klabu hiyo msimu huu 2022/23.

SAKATA LA KAPOMBE KUSHINDWA KUCHEZA DHIDI YA YANGA JUZI….SIMBA WATOA TAMKO…WAMUWEKEA KINGA KOCHA MAKI… ILE ISHU YA FRAGA KURUDI SIMBA IKO HIVI AISEEE….CHAMA NA WENZAKE WATINGA CAF MAPEMA TU…KILICHOBAKI NI ‘SHOW SHOW’…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply