Habari za michezo

FT: SIMBA 3-0 GEITA GOLD…. OKRAH, PHIRI NA CHAMA WAFANYA YAO….’MZUNGUU’ BADO SANA..AINGIA NA ZALI…

admin August 17, 2022 6:06 pm


KLABU ya Simba imeanza vizuri kwenye ligi ya NBC mara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Geita Gold, mchezo ambao ulipigwa jioni hii katika dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo ambao ulionekana wa aina yake hasa kwa timu zote kuonesha soka safi la kushambulia kutafuta mabao.

Shangwe ziende kwa wachezaji wapya wa timu ya Simba ambapo leo wameonesha makali yao kwa kucheza kandanda safi na wengine kupachika mabao safi, mabao ya Simbaa yaliwekwa kimyani na Augustino Okrah ambaye lipiga free kick ambayo ilimshindinda kipa kwa Geita Gold na kutinga nyavuni.

Mpaka mapumziko Simba Sc ilikuwa mbele kwa bao 1-0,na baadae mshambuliaji wao mpya Moses Phiri kupachika bao kali ambalo liliwanyanyua mashabiki kwa furaha kwenye dimbaa la Benjamini Mkapa.

Simba Sc ilipata bao la tatu kupitia kwa kiungo wao mshambuliaji Clautos Chama ambaye alifunga kwa mkwaju wa penati namatokeo kusomeka Simba Sc kuibuka na Ushindi wa mnono wa 3-0.

BAADA YA KUACHWA NA AZAM FC…MUDATHIR YAHYA ACHUKUA MAAMUZI MAGUMU…AJIWEKA KANDO NA SOKA JUMLA JUMLA… KUWANIA LIGI YA MABINGWA AFRIKA KWA WANAWAKE…SIMBA QUEENS WAIZIDI KUTIKISA AFRIKA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply