Habari za michezo

BAADA YA KUACHWA NA AZAM FC…MUDATHIR YAHYA ACHUKUA MAAMUZI MAGUMU…AJIWEKA KANDO NA SOKA JUMLA JUMLA…

admin August 17, 2022 5:40 pm


Kiungo wa zamani wa Azam FC, Mudathir Yahya amedai anapumzisha mwili wake kipindi hiki ligi ikiwa inaendelea kwa kuwa karibu na familia yake.

Mudathir amefunguka hayo baada ya kumaliza mkataba na Azam FC ambaye amedumu kwa misimu 12 ndani ya timu hiyo na kutwaa taji moja la ligi.

Akizungumza Mudathir alisema: “Nina uwezo wa kucheza msimu huu kwani dirisha bado halijafungwa na nimepata ofa kutoka timu mbalimbali ambazo nimezifahamisha kuwa nahitaji kupumzika kwa muda hadi dirisha dogo litakapofunguliwa.

“Naifahamu vizuri ligi ya Tanzania kwani nimecheza muda mrefu zaidi kuachwa na Azam FC haina maana kwamba kiwango changu kimeshuka nipo vizuri na naweza kucheza timu yopyote ambayo inaweza kunisajili.”

Mudathir alisema pamoja na kuamua kupumzika atakuwa anafanya mazoezi binafsi ili kujiweka fiti ili atakapoamua kurudi uwanjani asiwe na kazi kubwa ya kufanya hasa kupunguza mwili.

“Unajua mtu akiamua kupumzika anaweza akawa anakula na kulala muda mwingi, ni rahisi kuongeza mwili na kilo kuongezeka hivyo kwa mchezaji inaweza kuwa shida. Sitaki kukutana na changamoto hiyo nitafanya mazoezi kama kawaida,” alisema nyota huyo aliyedumu muda mrefu Azam FC.

BAADA YA YANGA KUUWASHA MOTO JANA…INJINI HERSI ATO TAMBO ZA KIBABE KWA SIMBA … FT: SIMBA 3-0 GEITA GOLD…. OKRAH, PHIRI NA CHAMA WAFANYA YAO….’MZUNGUU’ BADO SANA..AINGIA NA ZALI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply