Home Habari za michezo BAADA YA KUONYESHA KIWANGO CHA KUFA MTU…AZIZ KI APANDA CHEO YANGA….SASA RASMI...

BAADA YA KUONYESHA KIWANGO CHA KUFA MTU…AZIZ KI APANDA CHEO YANGA….SASA RASMI MAJUKUMU YAKE MAPYA NI HAYA…


Imefahamika kuwa Kiungo mshambuliaji kutoka Burkina Faso Stephen Aziz Ki amekabidhiwa jukumu maalum la kupiga mipira iliyokufa kwenye kikosi cha Young Africans, ambacho kina kazi kubwa ya kutetea ubingwa msimu huu.

Kiungo huyo aliyesajiliwa Jangwani majuma matatu yaliyopita, ameonekana akifanya kazi hiyo katika michezo yote aliyocheza, hali ambayo imeibua maswali kwa wadau wengi walioifuatilia Young Africans ikicheza kuanzia Tamasha la Kilele cha Wiki ya Mwananchi.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya Young Africans kimeeleza kuwa, Kiungo huyo aliyetamba na ASEC Mimosas ya Ivory Coast kabla ya kutua klabuni hapo, amekabidhiwa jukumu hilo maalum na Benchi la Ufundi linaloongozwa na Kocha Nabi.

Amesema tangu aliposajiliwa Aziz Ki na alipoonekana ana uwezo mkubwa wa kutimiza jukumu la kupiga mipira iliyokufa akiwa mazoezini, ndipo ilikua chanzo cha kupewa kazi hiyo.

“Aziz Ki ndiye mchezaji aliyeteuliwa kupiga mipira yote ya kona na faulo zitakazotokea katika michezo yetu, kama yeye atakuwa sehemu ya kikosi.”

“Kama ikitokea amepigwa mchezaji mwingine labda iwe kwa dharura, lakini huyo ndiye mchezaji aliyependekezwa kupiga mipira hiyo,” kimesema chanzo cha kuaminika ndani ya Young Africans

Hata hivyo alipoulizwa Kocha Nabi baada ya mchezo wa juzi Jumanne dhidi ya Polisi Tanzania Jijini Arusha, alisema mchezaji huyo ana uwezo wa kipekee wa kutimiza jukumu la kupiga mipira hiyo.

Alisema haimaanishi kama Aziz Ki ndio bora kuliko wengine, lakini umakini wake wa kutimiza jukumu alilokabidhiwa, ndio kulimsukuma kumpendekeza kiungo huyo.

“Wachezaji wangu wote wana uwezo wa kupiga mipira hiyo, lakini Aziz Ki ndiye aliyeteuliwa kutokana na uwezo wake wa kupiga vizuri zaidi.” amesema Kocha Nabi

Tangu aliposajiliwa klabuni hapo Aziz Ki ameshacheza michezo miwili ya ushindani dhidi ya Simba SC (Ngao ya Jamii) na juzi alicheza mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Polisi Tanzania, huku kwa mara ya kwanza akionekana machoni mwa mashabiki wa Young Africans wakati wa mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Mabingwa wa Uganda Vipers SC.

SOMA NA HII  CARLINHOS ATAMBA KUENDELEA KUUWASHA MOTO YANGA