Habari za michezo

PAMOJA NA YANGA KUCHEZA ARUSHA LEO…SIMBA WAIPIGA BAO KWA UPANDE WA JEZI…ZAGOMBANIWA KWA NJUGU….

admin August 20, 2022 12:20 pm

Licha ya jezi za Yanga kutawala kuelekea mchezo wa timu hiyo dhidi ya Coastal Union leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid hapa jijini Arusha, jezi za Simba zimeoneoka kuzipiga bao kwa bei.

Sasa kuelekea mchezo huo jezi za Yanga ndizo zimeonekana kutawala sana nje ya uwanja huo lakini zikipigwa bao na za watani zao Simba ambazo licha ya uchache lakini bei yake hazishikiki.

Jezi za Yanga mpya zinauzwa bei tofauti zile za njano na kijani ni Sh35000 ambayo ni bei elekezi huku nyeusi zikiuzwa Sh50,000 wakati jezi mpya za Simba zinauzwa Sh60,000.

Mmoja wa wauza jezi uwanjani hapo ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema jezi za Simba ndio zinauzika zaidi kwa kufuatiwa na za Yanga lakini pia chache za Coastal Union ambazo zipo uwanjani hapo.

“Unajua jezi za Yanga zimetoka nyingi tofauti na Simba hivyo  hata bei yake siyo kubwa sana lakini kama hapa unaona ya Simba ni moja tu lazima mtu atanunua kwa garama yoyote.” amesema.

HUYU HAPA STAA WA YANGA ANAYETAKIWA NA MARSEILLE YA UFARANSA…MWINYI ZAHERA TOA LA MOYONI KUHUSU DILI HILO.. JAMA JAMA ..HAWA AZAM FC HAWATAKI MZAHA MSIMU HUU….WAMESHUSHA KOCHA LINGINE LA KUTISHA…ALIKUWA FC PORTO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply