Azam FC

JAMA JAMA ..HAWA AZAM FC HAWATAKI MZAHA MSIMU HUU….WAMESHUSHA KOCHA LINGINE LA KUTISHA…ALIKUWA FC PORTO…

admin August 20, 2022 2:30 pm


Klabu ya Azam imemtambulisha rasmi, Joao Rodrigues raia wa Ureno kuwa mtaalamu wao mpya wa tiba za wachezaji (physiotherapist).

Rodrigues ametua usiku wa kuamkia leo Jumamosi ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho kinachotaka kufanya vizuri msimu huu.

Rodrigues ni mtaalamu wa viwango vya juu kwenye tiba za wachezaji, akiwahi pia kufanya kazi na mabingwa wa Ureno, FC Porto.

Mmiliki wa timu hiyo, Yusuf Bakhresa kabla ya kuanza msimu huu aliahidi atawapa furaha mashabiki wake kwa kuleta wachezaji wa hali ya juu, kocha wa viungo, kocha wa makipa na sasa amemaliza kwa kushusha ‘physio’ wa viwango.

Baada ya ujio wake sasa benchi la ufundi la timu hiyo litakuwa chini ya Kocha wake Mkuu, Abdihamid Moallin, Omary Nasser, ambaye ni Msaidizi, kocha wa washambuliaji, Kali Ongala, kocha wa viungo, Mikel Guillen na kocha wa makipa, Dani Cadena.

PAMOJA NA YANGA KUCHEZA ARUSHA LEO…SIMBA WAIPIGA BAO KWA UPANDE WA JEZI…ZAGOMBANIWA KWA NJUGU…. BARCELONA WAZIDI KUFULIA KIUCHUMI…MASTAA WADAI MALIMBIKIZO YA MISHAHARA …MCHEZAJI MADRID AWANANGA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply