Geita Gold FC

ILE ISHU YA USAJILI WA MJAPAN KWA GEITA GOLD ..MAMBO YOTE YAKO HIVI KUMBE…MINZIRO AFUNGUKA A-Z UKWELI WA MAMBO…

admin August 25, 2022 9:05 am


Kocha Mkuu wa Geita Gold, Fred Felix Minziro, amesema wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha vibali vya nyota wao, Shinobu Sakai raia wa Japan, tayari kwa kuanza kumtumia kwenye mechi za Ligi Kuu na mashindano mengine.

Geita Gold ambayo inajiandaa na mashindano ya kimataifa ni miongoni mwa timu za Ligi Kuu zilizosajili nyota wa kimataifa kwa lengo la kuleta ushindani.

Akizungumza, Minziro alisema, anaimani kubwa na Mjapan wake pindi atakapoanza kuitumikia timu hiyo, na kudai kuwa wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha vibali vyake vya kufanya kazi nchini ili kuanza kutumika.

“Tupo katika hatua za mwisho za kukamilisha vibali vya mchezaji wetu Shinob, hakuweza kucheza mechi za awali kwa kuwa hakuwa na kibali cha kazi na makazi, hivyo tunakamilisha utaratibu ili aweze kucheza.

“Ninamatumaini makubwa akianza kucheza kikosi kitakuwa kizuri pale atakapozoeana na wachezaji wenzake, lengo letu tunahitaji kuwa na kikosi bora cha ushindani msimu huu kuliko ulivyokuwa msimu uliopita,” alisema Minziro.

ZA NDAANI KABISA…WAKATI MASHABIKI WAKIMSUBIRI KWA HAMU….DILI LA MANZOKI KUTUA SIMBA LAOTA MBAWA…UKWELI HUU HAPA… KUHUSU KELELE ZA MASHABIKI KUWA YEYE NI ‘NYOKA LA KIBISA’….AZIZ KI AVUNJA UKIMYA…NABI AKAZIA ALIYOYASEMA …

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply