Habari za michezo

BAADA YA KUONA YANGA KAMA WAMEMSUSA HIVI….YACOUBA ACHUKUA UAMUZI HUU…ADAI ANAPITIA KIPINDI KIGUMU…

admin August 26, 2022 3:03 am


Hatimaye Kiungo mshambuliaji wa Yanga Yacouba Songne amerejea kwao Burkinafaso kwa matibabu zaidi.

Yacouba ambae ameuguza majeraha kwa muda mrefu sasa baada ya kuumia mwanzoni mwa msimu uliopita bado ana mkataba na kalabu ya Yanga na alitajwa kutolewa kwa mkopo ili akapate nafasi ya kurudisha kiwango chake.

Yacouba alihusishwa na timu nyingi, huku Geita Gold ikionekana ndipo ambapo atakwenda staa huyo.

Lakini ghafla mambo yamebadilika na sasa Staa huyo amerejea kwa Burkinafaso.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagrama Yacouba ameandika;

“Msiwe na wasiwasi, kwa sasa napitia kwenye wakati mgumu lakini nitakuwa imara tena”

Yacouba amepewa program maalumu ambayo ataendelea kuitekeleza wakati wote akiwa nyumbani kwao Burkinafaso.

Yacouba hajaorodheshwa kwenye list ya majina ya Wachezaji wa Yanga msimu wa (2022/23) lakini ataendelea kuwa mchezaji wa Yanga.

WAKATI ONYANGO AKISEMEKANA KUTOKUWA NA FURAHA SIMBA….KOCHA MAKI AIBUKA NA HILI JIPYA LINALOMUHUSU… WAKIJUA WATACHEZA NA SIMBA HIVI KARIBUNI…KMC WAANZA  MBWEMWE HIZI ZA HATARI…WAPANGA KUJA KWA STAILI MPYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply