Habari za michezo

KUHUSU ISHU YA KURUDI TENA BONGO….NIYONZIMA AANIKA JINSI VIGOGO WA SOKA BONGO WANAVYOMPAPATIKIA…

admin August 30, 2022 2:47 am


Kiungo aliyewahi kutamba na Yanga pamoja na Simba, Haruna Niyonzima amekiri kufuatwa na timu za Ligi Kuu Tanzania Bara ambazo zimetaka huduma yake, lakini Mnyarwanda huyo akazichomolea.

Timu ambazo zimekuwa zikihusishwa kusakata ni pamoja na Singida Big Stars na Geita Gold, ambapo Niyonzima amesema;

“Ni kweli timu zaidi ya mbili zilinitafuta zikitaka huduma yangu lakini hatukuweza kufikia makubaliano kutokana na maslahi binafsi.

“Ujue mpira ndio unaendesha maisha na faimilia yangu mali nilizonazo zote zimetokana na mpira hivyo lazima niuheshimu na kuwa na mipaka ya maslahi nadhani hiyo ndio sababu kuu ya dili hizo kutokamilika,”

Niyonzima ameongeza kuwa hajachuja kiwango kutokana na nidhamu, malengo na kujituma kwake mazoezini na uwanjani. Sasa anakipiga timu ya AS Kigali ya Rwanda, pia ni nahodha wa Rwanda (Amavubi)

KUHUSU MICHUANO YA CAF…ALEX SONG AIPIGIA ‘UPATU’ SIMBA…AFUNGUKA MATAMANIO YAKE YA MOYONI….. WAKATI TAARIFA ZA ‘VIJIWENI’ ZIKISEMA KOCHA SIMBA ANAWACHUKIA  CHAMA NA PHIRI…KUMBE UKWELI WA MAMBO UKO HIVI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply