Habari za michezo

MWAMUZI COASTAL VS YANGA YAMKUTA YAKUMKUTA….’ALIMWA RUNGU LA KICHWA’ MAZIMA MAZIMA…

admin August 30, 2022 4:08 pm


Mwamuzi wa kati aliyesimamia mchezo baina ya Coastal Union na Young Africans SC, Raphael Ikambi kutoka mkoani Morogoro ameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitatu baada ya kutenda kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu.

Kwa mujibu wa KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Ikambi alishindwa kufanya maamuzi sahihi kwa mujibu wa sheria za mpira wa miguu katika tukio ambalo mchezaji wa Coastal Union, Mtenje Albano alimchezea mchezo hatarishi na usio wa kiungwana mchezaji wa Young Africans, Yanick Bangala ambaye baada ya tukio hilo aliinuka na kwenda kumsukuma Mtenje Albano.

Adhabu hii ni kwa uzingativu wa Kanuni ya 42:1(1.1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi. Yanga SC ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa goli 0-2 dhidi ya wenyeji wa mchezo Coastal Union.

SIKU MOJA BAADA YA AZAM KUMFUKUZA KOCHA WAO MSOMALI…’BWALYA’ WA SIMBA AWASHUSHIA LAWAMA WACHEZAJI.. NI YANGA TENA….TFF WAIKAMUA MAMILIONI YA SHILINGI…ISHU NZIMA IKO NAMNA HIVI AISEE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply