Home Habari za michezo BAADA YA UKIMYA MWIINGII….HATIMAYE ZAHERA AVUNJA UKIMYA YANGA…ATAJA TATIZO LA SOKA LA...

BAADA YA UKIMYA MWIINGII….HATIMAYE ZAHERA AVUNJA UKIMYA YANGA…ATAJA TATIZO LA SOKA LA TZ

 


MKURUGENZI wa Ufundi wa Yanga, Mwinyi Zahera, amezitaka klabu zote hapa nchini kutengeneza wachezaji vijana kwa ajili ya kuwaandaa kuwa wanasoka nyota wa baadaye na si kubakia katika vita ya kushinda vikombe pekee.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Zahera, alisema amekuwa akiwatengeneza wachezaji vijana chini ya miaka 17 na miaka 20 kwa ajili ya kuwabadilisha na kuwa wachezaji wenye uwezo na maarifa makubwa.

“Soka la vijana ni kama shule, huko kuna wa kwanza hadi wa mwisho huku walimu wakiangalia namna ya kuwaendeleza wale walio juu na kuwarekebisha waliko chini ili nao viwango vyao vipande.

“Hakuna klabu ambayo inatengeneza wachezaji wa umri chini ya miaka 17 na miaka 20 wote waje kuwa nyota, ndiyo maana unaona timu nyingi kubwa duniani zina wachezaji vijana, lakini si wote wanaokwenda kuchezea timu kubwa au kuwa nyota,” alisema Zahera.

Aliongeza naye anawatengeneza wachezaji katika klabu hiyo kwa mfumo huo na anazikumbusha timu nyingine kufuata nyayo hizo badala ya kujipanga  kushinda mataji pekee.

“Na hata mazoezi ninayowapa, hatufanyi kwa ajili ya kuchukua ubingwa, ni yale ya kuwajenga watoto na kuwapata hata wawili watatu ambao wanaweza kwenda timu kubwa, hiyo falsafa ya mafunzo kwa wachezaji vijana duniani kote,” alisema Mkongomani huyo.

SOMA NA HII  YANGA WAITIA TUMBO JOTO SIMBA, VIONGOZI WAHAHA