Home Habari za michezo FT: COASTAL UNION 0-2 YANGA SC…MAYELE KAMA KAWA AENDELEZA ALIPOISHIA…MORRISON AANZA KUWAKERAAAH….

FT: COASTAL UNION 0-2 YANGA SC…MAYELE KAMA KAWA AENDELEZA ALIPOISHIA…MORRISON AANZA KUWAKERAAAH….


Kama walivyomaliza Ligi ndivyo walivyoanza msimu huu baada ya hii leo Klabu ya Yanga kuitandika Coastal Union magoli 2-0 ugenini mchezo wa Ligi Kuu ya NBC 2022/2023.

Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Sheikh Amri abeid, umewashuhudia Yanga wakianza na mabadiliko katika kikosi chao kwa kutokuwa na golikipa Djigui Diarra, Beki Dickson Job huku Fiston Mayele akianzia benchi.

Iliwachukua Yanga dakika 4 tu kujiandikia bao la uongozi kupitia kwa Bernard Morisson.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Yanga walikua kifua mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili Yanga walirudi kwa kasi huku wakicheza soka safi na dakika ya 67 Fiston Mayele alieingia akitokea benchi akawahakikishia Wananchi alama tatu kwa bao lake la kichwa.

Mpaka sasa Fiston Mayele amecheza michezo miwili na kufunga magoli mawili.

Kwa ushindi huo Yanga wanakwenda kileleni katika msimamo wa Ligi wakiwa na alama 6.

SOMA NA HII  HIZI HAPA SABABU 5 KUNTU KWA NINI MSUVA ATAJIUNGA NA YANGA NA KUIPIGA CHINI SIMBA...