Home Geita Gold FC KISA KUANZA LIGI KWA KICHAPO KIZITO KUTOKA SIMBA NA SARE DHIDI YA...

KISA KUANZA LIGI KWA KICHAPO KIZITO KUTOKA SIMBA NA SARE DHIDI YA AZAM…MNZIRO AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA HAYA…


Kocha Mkuu wa Geita Gold FC Fred Felix Minziro amesema michezo miwili ya Ligi Kuu dhidi ya Simba SC na Azam FC imempa nafasi ya kutambua ubora na udhaifu wa kikosi chake msimu huu 2022/23.

Geita Gold FC ilianza Msimu kwa kupoteza 3-0 dhidi ya Simba SC, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, kisha kulazimisha sare ya 1-1 dhidiya Azam FC, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Minziro amesema michezo hiyo aliyochezwa ugenini imemuwezesha kutambua namna atakavyoendelea kupambana msimu huu, ili kufanikisha lengo la kumaliza katika nafasi za juu kwenye msimamo, kama ilivyokua msimu uliopita 2021/22.

Amesema michezo hiyo ilikua kipimo kizuri kwa wachezaji wake, na imekua chachu katika Benchi lake la Ufundi kuanza kuyafanyia kazi mapungufu yaliyoonekana huku wakiboresha mazuri yaliyojitokeza.

“Nimepata kipimo kizuri na bora kwa sababu tunakabiliwa na Michezo mingi ya Ligi Kuu, pia tutashiriki Michuano ya Kimataifa kuanzia mwezi ujao, imekua chachu kwangu na kwa wenzangu wa Benchi la Ufundi kutambua wapi tumekosea na wapi tuongeze bidii kwa ajili ya kuendeleza mazuri tulioyapata.”

“Tumecheza na timu Nzuri na Bora katika Ligi Kuu, zimetupa upinzani wa kutosha kwa sababu tumepoteza mchezo mmoja na kupata matokeo ya sare, sio matokeo mabaya kwa sababu tumeanzia ugenini,”

“Baada ya kupoteza dhidi ya Simba SC nilikaa na wachezjai wangu na kuwaambia tumepoteza kwa idadi kubwa ya mabao, nashukuru Mungu walinisikiliza na kupambana kwenye mchezo dhidi ya Azam FC, tukapata alama moja.”

“Muda huu wa majuma mawili hapa tutautumia kujiandaa vizuri kwa kuangali udhaifu uliotufanya kuanza vibaya Ligi Kuu, ninaamini maandalizi haya yatatusaidia sana hadi kwenye Michuano ya Kimataifa.” amesema Kocha Minziro.

Geita Gold FC itacheza Mzunguuko wa tatu wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Septemba 06.

Septemba 09 Geita Gold itaingia kwenye Mshike Mshike wa Michuano ya Kimataifa ambapo watakipiga dhidi ya Hilal Alsahil SC itakayoanzia nyumbani Sudan, kabla ya kuja Tanzania kwa mchezo wa Mkondo wa Pili utakaounguruma Septamba 16.

SOMA NA HII  KOCHA WA ASEC MIMOSAS AKUBALI KUWAACHIA YANGA KIFAA HIKI...WARABU WANATAMBUA JOTO LAKE...