Home Azam FC KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA….GEITA GOLD WAPEWA MIFUPA MIGUMU TUPU…AZAM WAPEWA WAARABU WEUSI...

KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA….GEITA GOLD WAPEWA MIFUPA MIGUMU TUPU…AZAM WAPEWA WAARABU WEUSI TUPU…


Matajiri wa madini, Klabu ya Geita Gold imepangwa kukutana na timu ya Hilal Al Sahil ya Sudan Kaskazini katika mechi ya hatua ya awali raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Katika raundi ya pili ya mtoano, mshindi kati ya Geita Gold na Hilal Al Sahil atakutana na Pyramids FC ya Misri.

Matajiri wa jiji la Dar, Azam FC ambao wanaanzia katika hatua ya pili ya mtoano katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, wamepangwa kukutana na mshindi kati ya Al Akhder ya Libya na Al Ahli Khartoum ya Sudan Kaskazini.

Al Akhder na Al Ahli Khartoum watakipiga katika raundi ya kwanza ya mtoano ambapo mshindi kati yao ndiye atakutana na Azam katika hatua inayofuata.

Mechi za kwanza za raundi ya kwanza zitapigwa Septemba 9, 10 na 11, mwaka huu 2022 wakati mechi za marudiano raundi ya kwanza zitapigwa Septemba 16, 17 na 18 mwaka huu.

Adha, michezo ya kwanza raundi ya pili ya mtoano itapigwa Oktoba 7, 8 na 9 mwaka huu 2022 wakati mechi za marudiano za raundi ya pili ya mtoano zitapigwa Oktoba 14, 14 na 16, mwaka huu.

SOMA NA HII  AZAM FC:MSIMU HUU USHINDANI NI MKUBWA