Home BIashara United PAMOJA NA KUCHAPWA MPAKA AKACHAKAA JUZI…MANDONGA AMTAKA DULLAH MBABE…AMTOLEA MANENO YA ‘SHOMBO’…

PAMOJA NA KUCHAPWA MPAKA AKACHAKAA JUZI…MANDONGA AMTAKA DULLAH MBABE…AMTOLEA MANENO YA ‘SHOMBO’…


Licha ya kuchapwa kwa Knock Out, Karim Mandonga amedai anatamani kucheza na bondia, Abdallah ‘Dullah Mbabe’ Pazi pambano lake lijalo.

Amesema ni bondia ambaye huwa anatamani kuzichapa naye kwa muda mrefu na anaamini atampa upinzani.

“Natamani kucheza na Dullah Mbabe, naamini kuna siku hili litatimia,” alisema bondia huyo ambaye usiku wa kuamkia juzi Jumapili alichapwa kwa KO na Shaaban Kaoneka huku akitoboa siri ya kipigo hicho na kuwaomba mashabiki wake kutorudi nyuma.

“Mpinzani wangu alinipiga right (ngumi ya kulia) akaunganisha na left hook, nikayumba, wakati natambalia mikono nikitaka kunyanyuka refarii akamaliza pambano,” alisema Mandonga mtu kazi.

Alisema Mandonga mtu kazi yuko fiti na mashabiki wake wasirudi nyuma kwani kukosea leo sio kukosea kesho.

“Michezo yetu ni ya makosa, ukifanya kosa moja mwenzako anatumia kukumaliza, ndicho kilichotokea kwangu,” alisema Mandonga. Bondia huyo alichapwa na Kaoneka raundi ya nne ya pambano lililopigwa mjini Songea usiku wa kuamkia jana.

“Nilijitahidi sana kupambana, lakini jitihada zangu ziliishia pale, lakini matokeo yale hayatanirudisha nyuma, sasa nataka kuzichapa na watu wenye rekodi bora kwenye ngumi, hasa wakongwe.

“Nikirudi Dar es Salaam naenda kupiga kambi na mabondia wa Ngome nikajifue jeshini, hivyo atakayefuata kazi anayo,” alisema.

Kuhusu tambo zake zilizomtambulisha zaidi kwenye ndondi, Mandonga amesema kila mmoja Mungu kamuandaa na kumpa kipaji chake.

“Mimi Mungu kaniandaa hivi na nafsi yangu ilishakubali kupambana katika mchezo huu ,” alisema bondia huyo anayepigania uzani wa super middle.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUFUNGWA 4-1.....MTIBWA WATAKIWA KUSHURUKURU MUNGU KWA KIPIGO HICHO..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here