Home Habari za michezo TETESI ZA USAJILI ULAYA: CHEALSEA WAIVIMBIA BARCELONA KWA AUBAMEYANG…WAKATAA KUTOA MZIGO WOTE…

TETESI ZA USAJILI ULAYA: CHEALSEA WAIVIMBIA BARCELONA KWA AUBAMEYANG…WAKATAA KUTOA MZIGO WOTE…

Klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza ipo mbioni kukamilisha usajili wa wachezaji Pierre Emerick Aubameyang kutoka Barcelona pamoja na mlinzi wa kati wa Leicester City Wesley Fofana.


Taarifa za ndani zimebainisha kuwa usiku wa kuamkia leo wakala wa Aubameyang alikutana na uongozi wa Barcelona kujadili uwezekano wa kumruhusu mteja wake kurudi tena jijini London kujiunga na Chelsea.

Licha ya kuonesha nia ya kumnasa Aubameyang, Chelsea imebainisha kuwa ipo tayari kutoa kiasi cha Paundi milioni 15 tu na siyo 30 ambayo Barcelona wameripotiwa kuihitaji ili kumuachia Aubameyang.

Upande wa Wesley Fofana, kocha mkuu wa Leicester City Brendan Rodgers ameweka wazi kuwa mlinzi wake hawezi kuhusika kwenye mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Southampton kutokana na kutokuwa sawa baada ya ofa mbili kutoka Chelsea kukataliwa na klabu hiyo.

Dirisha la usajili linatarajiwa kufungwa Agosti 31 huku zikiwa zimebaki siku 11 tu ambapo mambo mengi kuhusu usajili yanaendelea kushika vichwa vya Habari pamoja na mitandao ya kijamii kote duniani.

Aidha sambamba na Fofana na Aubameyang Chelsea pia imeonesha nia ya kumsajili winga wa Everton Anthony Gordon ingawa kocha wake Frank Lampard ameibuka na kusema kuwa mchezaji huyo hauzwi na ni mali ya Everton
SOMA NA HII  KIGOGO WA SUPER LEAGUE AKOMAA