Home Habari za michezo UKWELI KUHUSU OKWA KUTUA BONGO BADALA YA MISRI WALIKO SIMBA UKO HIVI….MAMBO...

UKWELI KUHUSU OKWA KUTUA BONGO BADALA YA MISRI WALIKO SIMBA UKO HIVI….MAMBO YAPELEKWA KIMYA KIMYA …


Kiungo mshambuliaji raia wa Nigeria, Nelson Esor Okwa tayari amewasili Tanzania usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Simba Sc.

Okwa ambaye alikuwa akikipiga katika Klabu ya Rivers United amewasili kwa ndege ya Shirika la Ethiopian Airlines na kufichwa kwenye moja ya hoteli iliyopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Okwa baada ya kuwasili asubuhi ya leo Jumatano atakamilisha taratibu zake za kujiunga na Simba na huenda muda wowote akatambulishwa kama mchezaji mpya wa kikosi hicho.

Baada ya Okwa, Simba pia inatarajia kumsajili mshambuliaji mwingine wa kigeni ambapo Cesar Manzoki wa Vipers ya Uganda anatajwa.

Ikumbukwe wakati wa uzinduzi wa wiki ya Simba CEO, Barbara Gonzalez alisema hawajakamilisha kutangaza wachezaji waliowasajili.

SOMA NA HII  KUHUSU BALEKE KUSAJILIWA KWA MKOPO...BOSI SIMBA AVUNJA UKIMYA...AFUNGUKA MKATABA ULIVYO...