BONDIA kutoka Tanzania Hassan Mwakinyo leo Septemba 3,2022 anatarajiwa kupanda ulingoni kuzichapa kwenye pambano la raundi 12.
Jana Septemba 2, Mwakinyo aliweza kupima uzito huko jijini Liverpool nchini Uingereza akiwa tayari kushuka Ulingoni kuzichapa na Muingereza Liam Smith.
Pambano hilo linatarajiwa kuchezwa saa 3:00 usiku Jijini Liverpool kwenye Ukumbi wa M&S Bank Arena ndani ya jiji hilo.
Katika zoezi hilo la upimaji uzito Mwakinyo alionekana kutokuwa na wasiwasi wowote mbele ya mpinzani wake Smith walipokuwa wakitazamana uso kwa uso.
Pambano hilo ni la uzani wa Super Walter, ambapo Mwakinyo alibainisha kuwa yupo tayari kwa ajili ya pambano la leo.