Habari za michezo

UGANDA vs TANZANIA : KAZI BADO MBICHI LEO…STARS WAPANIA KUTIA MCHANGA ‘PILAU’ LA WAGANDA…

admin September 3, 2022 10:35 am

BADO kazi haijaisha kwa wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ ambao leo wanatarajiwa kutupa kete ya pili kwenye mchezo wao wa pili dhidi ya Timu ya Taifa ya Uganda.

Dakika 90 za mwanzo zilikuwa na maumivu hasa baada ya Stars kuambulia kichapo cha bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa nyumbani matumaini yalikuwa makubwa kwa kila mmoja kuamini kwamba timu inaweza kushinda kuongeza nguvu kwenye tiketi ya kuwania kufuzu CHAN.

Haikuwa hivyo na mwisho kila mmoja alitoka akiwa na lake moyoni kutokana na Stars kupoteza wakiwa nyumbani katika dakika za lala salama.

Ipo hivyo mchezo wa mpira ni makosa pale ambapo Stars walifanya makosa wapinzani wao Uganda walitumia kuwaadhibu na sasa wanakwenda kwenye mchezo mwingine ambao wana nafasi ya kushinda.

Haitakuwa kwa wepesi ukizingatia benchi la ufundi ni jipya baada ya Kim Poulsen kuondolewa na presha kwa kila mmoja inaonekana kuwa juu.

Inawezekana kuna kitu kitaonekana kwa wachezaji leo lakini kinachotakiwa ni kila mmoja kujituma bila kuogopa kwenye mchezo wa leo.

Watanzania Stars ni yetu na kila mmoja anajukumu la kuongeza kuomba dua ili matokeo yawe chanya watakaporejea tukawapokee mashujaa wetu wakiwa na jambo la tofauti wametuletea.

Itakuwa hivyo wachezaji wakijituma na kuamini kwamba kama wao waliweza kushinda wakiwa ugenini basi dakika 90 zitakuwa zao wakiwa ugenini pia.

KWA MARA YA KWANZA TOKA AJIUNGE YANGA….KISINDA AFUNGUKA A-Z KILICHOMTOA MOROCCO… FT: SIMBA SC 0-1 ARTA SOLAR….GOLI LAO LAFUNGWA NA MTANZANIA…’STRAIKA MZUNGU’ AZIDI KUPEPESUKA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply