Burudani

ISHU YA MWAKINYO KUPIGWA JANA…MJADALA WA KUUZA MECHI WAIBUKA…MASHABIKI UINGEREZA WAMTOLEA ‘POVU’…

admin September 4, 2022 9:15 am


Mara baada ya Hassan Mwakinyo kushuhudiwa akipigwa kwa TKO na bondia Liam Smith, mijadala mbalimbali imeibuka katika mitandao ya kijamii.

Lakini mjadala mkubwa ni ule ambao, wengi wamekuwa wakijiuliza Je, Mwakinyo alilipwa pesa ili auze mchezo wake kwa kumpa ubingwa bondia huyo ambaye katika mchezo huu alikuwa ni Mpinzani wake?

Mmoja kati ya watu waliohoji kuhusiana na hili ni meya wa zamani wa Ubungo Boniface Jacob ambaye ameandika kupitia ukurasa wake wa twitter akisema 

“Sasa hii Mwakinyo ataniambia nini niamini kwamba hajauza game?”

Hii inakuja kutokana na kiwango ambacho Hassan Mwakinyo alikionyesha katika mchezo tangu mzunguko wa kwanza wa pambano hilo ulipoanza hadi pale matokeo yaliyowaacha watanzania wengi midomo wazi yalipojitokeza.

Mbali na hivyo, mashabiki mbalimbali nchini Ungereza wametoa maoni yao kwenye mtandao wa Sky Sports wakionyeshwa kuchukizwa na kiwango cha Mwakinyo, huku wakifika mbali kutaka asipewe tena nafasi ya kupigana nchini huko.

Mashabiki hao walisema kuwa ni ngumu kuamini pambano hilo walilotaraji kuwa lingekuwa kali na la aina yake kumalizika kwa staili ya namna ile.

Je, nini mtazamo wako kuhusiana na mjadal huu unaohusu Mwakinyo kuuza mchezo wake wa usiku huu wa leo?

BAADA YA TAIFA STARS KUFUNGWA JANA…FEI TOTO AONYESHA RANGI YAKE HALISI…AIBUKA NA KAULI HII KWA WATZ… PAMOJA NA KUKOSA MAGOLI YA WAZI JANA….STRAIKA MZUNGU WA SIMBA AZIDI KULIKOROGA…ATOA UJUMBE HUU MKALI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply