Habari za michezo

BAADA YA TAIFA STARS KUFUNGWA JANA…FEI TOTO AONYESHA RANGI YAKE HALISI…AIBUKA NA KAULI HII KWA WATZ…

admin September 4, 2022 9:05 am


Kiungo mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amewaomba radhi Watanzania na mashabiki wote wa mpira kufuatia kichapo cha Stars kutoka kwa Timu ya Taifa ya Uganda.

Katika mchezo huo wa marudiano kuwania kufuzu fainali za Kombe la CHAN, ulipigwa nchini Uganda, Stars ilipigwa bao 3-0 na kuondoshwa rasmi katika michuano hiyo.

Mchezo wa kwanza uliopigwa weekendbiliyopita, Stars ilifungwa bao 1-0 na Uganda, hivyo Tanzania imeondoshwa kwa kufungwa na Uganda jumla ya bao 4-0 katika michezo miwili.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Fei Toto ameandika; “Watanzania wenzangu, najua inaumiza, najua inakera, najua maumivu mnayoyapitia sababu mnapenda kuiona timu yetu ya taifa ikifanya vizuri.

“Tulipewa jukumu la kuibeba bendera ya taifa letu tumewaangusha. Nichukue fursa hii kuwaomba radhi, naamini tutafanya vizuri hapo mbeleni,” amesema Fei Toto.

BAADA YA DIRISHA LA USAJILI KUFUNGWA….MASTAA WA KICONGO WAJAZANA ZAIDI YANGA…TAKWIMU HIZI HAPA… ISHU YA MWAKINYO KUPIGWA JANA…MJADALA WA KUUZA MECHI WAIBUKA…MASHABIKI UINGEREZA WAMTOLEA ‘POVU’…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply