Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA SIMBA….HITIMANA AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA KUCHOSHWA NA UTUMWA WA TIMU KUBWA…

KUELEKEA MECHI NA SIMBA….HITIMANA AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA KUCHOSHWA NA UTUMWA WA TIMU KUBWA…


Kocha Mkuu wa KMC, Thierry Hitimana amesema ni muda sahihi kwake wa kukata minyororo ya unyonge kwa kutaka kuvunja uteja uliotawala kwa timu yake dhidi ya Simba wakati zitakapovaana kesho kwenye mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Bara.

Timu hizo zinakutana kwenye mechi ya kwanza msimu huu ikiwa ni mchezo wa tatu wa kila mmoja tangu Ligi Kuu ilipoanza Agosti 15, pambano litakalochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku rekodi zikionyesha KMC haijawahi kushinda mbele ya Simba tangu ilipopanda daraja msimu wa 2017-2018.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Hitimana alisema kwa maandalizi aliyofanya katika kipindi hichi cha wiki mbili kupisha michezo ya kimataifa, anaamini kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mchezo huo huku akiwa na matumaini ya kushinda.

“Sio mchezo mwepesi kwa sababu kila tunapocheza na Simba wanatusumbua sana ingawa hiyo mentality (mawazo) nimeyatoa kwa wachezaji wangu, tumecheza mechi nyingi za kirafiki ambazo ni saizi ya Simba hivyo sina wasiwasi kabisa,” alisema kocha huyo kutoka Burundi na kuongeza;

“Siwezi kuweka wazi ubora au udhaifu wa wapinzani wetu kwa sababu hata wao pia wanatufuatilia, ila itoshe tu kusema tupo tayari kwa mchezo,” alisema Hitimana aliyekuwa msaidizi wa Didier Gomez kuanzia Septemba 11, mwaka jana kabla ya kuachana na klabu hiyo Desemba 28, 2021.

Kwa upande wa beki wa kikosi hicho, Ibrahim Ame ambaye pia amewahi kuichezea Simba alisema anawaheshimu wapinzani wao ila wasitarajie mteremko kwenye mchezo huo kwani yeye binafsi na wenzake wamejipanga vizuri kuhakikisha wanaibuka na ushindi. KMC haijawahi kupata ushindi ama kutoka sare mbele ya Simba katika Ligi Kuu katika michezo nane waliyokutana tangu msimu wa 2017-2018.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE