Habari za michezo

KIMEUMANA CHELSEA….TUCHEL NAYE ‘KALIWA KICHWA’ MCHANA HUU…

admin September 7, 2022 10:45 am


Hatimaye Uongozi wa Klabu ya Chelsea ya England umefikia makubaliano ya kuachana na Meneja wa kikosi chao Thomas Tuchel baada ya kuwa na muendelezo usioridhisha ndani ya klabu hiyo.

Klabu hiyo iliyo chini ya umiliki wa Mfanyabiashara wa Marekani na mmiliki wa kampuni ya Eldridge Todd Boehly na Cleaverlake imetoa taarifa juu ya kufikia makubaliano na Tuchel kuacha kuinoa klabu ya Chelsea.

“Wakufunzi wa Chelsea watasimamia timu kwa mazoezi na maandalizi ya mechi zetu zijazo huku Klabu ikipiga hatua kwa haraka kuteua kocha mkuu mpya,” imesema taarifa hiyo.

Raia huyo wa Ujerumani alirithi mikoba ya kuinoa Chelsea kutoka kwa Frank Lampard mwanzoni mwa mwaka 2021 huku akitwaa mataji makubwa barani ulaya ikiwepo Klabu bingwa barani Ulaya akiwa kocha wa pili kutwaa taji hilo baada ya kocha Roberto Di Mateo.

RASMI….TFF WAKUBALI KUKAA KIKAO KUJADILI ISHU YA KISINDA NA ONYANGO…HAKUMU ZAO KUSOMWA IJUMAA… ILI KUEPUSHA YASIJE KUJITOKEZA YA MWAKINYO….TWAHA KIDUKU APATA MBELEKO YA MBUNGE…MCHONGO MZIMA UKO HIVI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply