Habari za michezo

KUELEKEA MECHI YA CAF KESHO KUTWA…HATMA YA KAPOMBE NA MKUDE MIKONONI MWA MGUNDA….

admin September 8, 2022 5:36 pm


Shomari Kapombe na Jonas Mkude wameungana na kikosi katika safari ya kwenda kuvaana na Wamalawi, Nyasa Big Bullet.

Shomari na Mkude hawakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kilichocheza jana Septemba 7, 2022 dhidi ya KMC na Wekundu hao wa Msimbazi kutoka sare ya goli 2-2.

Kapombe, Mkude sambamba na Peter Banda wameonekana mapema hii kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere sambamba na nyota wengine wa timu hiyo, tayari kwa mechi hiyo ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa Septemba 10, 2022.

Simba wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa na Kocha Mkuu mpya Juma Mgunda waliyemtangaza kufanya naye kazi kwa muda baada ya kuachana na aliyekuwa kocha wao mkuu Zoran Maki.

BAADA YA KUIONA RANGI HALISI YA YANGA….STAA WA ZAMANI WA NEWCASTLE YA EPL KAAMUA KUFUNGUKA HAYA YA MOYONI… WAKATI WAKIJINDAA NA SINGIDA BIG STARS….MASUDI DJUMA KAJIPIGA PIGA KIFUANI ..KISHA KWA JEURI AKASEMA HAYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply