Habari za michezo

KLOPP ALIA MAMBO MAGUMU LIVERPOOL…KIPIGO CHA NAPOLI CHAIBUA MENGI MAZITO…

admin September 9, 2022 8:54 am


Kocha Mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp amekiri kwamba timu yake ya Liverpool inahitaji kujipanga upya baada ya kipigo cha goli 4 kwa 1 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Napoli.

Liverpool waliruhusu mabao matatu katika kipindi cha kwanza kabla ya kufungwa bao la nne katika hatua za mwanzo za kipindi cha pili. Luis Diaz aliifungia Liverpool bao la kufutia machozi, lakini timu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza haikuonekana kurejea mchezoni

Kikosi cha Klopp sasa kimeshinda mechi mbili pekee kati ya saba za kwanza za msimu huu, na kocha huyo wa Ujerumani anaamini mabadiliko makubwa yanahitajika ili kubadilisha mambo.

“Tulicheza vibaya katika kipindi cha kwanza lakini kwa kawaida huwa haturuhusu mabao matatu,

“Tuna Wolves Jumamosi na kama wameangalia mchezo usiku wa leo, hawawezi kuacha kucheka, watasema na sisi pia ni wakati mwafaka wa kuwacheza nao, lazima tujipange vizuri zaidi katika kila kitu,” alisema Klopp.

Klopp ameitaka timu yake kukaa chini na kutafuta suluhu ili kurejea katika ubora wao.

“Hatuchezi vizuri vya kutosha, hiyo ni dhahiri na ndiyo maana tunapoteza michezo, kuna kazi ya kufanya, ni jukumu langu na ninahitaji muda wa kufikiria. Kuna mambo machache dhahiri na inabidi tuyaweke.” Alisema klopp

BAADA YA KUONA ZORAN ALIVYOWAPELEKA PUTA SIMBA…AZAM FC WAAMUA KUMPA UKWELI HUU MAPEMA KOCHA WAO MPYA… SAKATA LA KISINDA…YANGA WAZIDI KUKOLEZA MOTO…WAENDELEA KUTUPA MADONGO TFF KWA NAMNA WALIVYOWAGEUKA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply