Habari za michezo

ACHANA NA RONALDO…HUYU HAPA STAA MWINGINE WA MAN UTD AMBAYE YUKO TOKA ENZI ZA FERGUSON…ANA ‘KIZIZI’ ..

admin September 10, 2022 9:15 am


Naweza kuamini kwamba kuna watu duniani wanaishi kwa janja janja , na wanaweza kupata kipato bila kufanya kazi.

Pale katika viunga vya Old Trafford ķuna huyu bwana mdogo anaitwa Philip Anthony Jones ambae ni kiraka wa kuhudumu nafasi kama tatu kwa uwezo wake.

Philip Jones alijiunga na Manchester 2010 akitokea katika klabu ya Blackburn Rovers kwa ada inayotajwa kufika Pauni milioni 16.5, kwa wakati huo Man United ikiwa chini ya Kocha Sir Alex Ferguson.

Ikiwa ni miaka 12 sasa tangu kitasa huyu kujiunga na Mashetani Wekundu, amecheza michezo 229 na kufunga Magoli 6.

Jones ni Mwanaume ambaye amenusurika kuuzwa na Ferguson, Moyes, Louis Van Gaal, Giggs, Mourinho, Ole, Carrick, Ralf na bado anaishi hadi leo bila kupata nafasi ya kucheza.

Kitu cha kufurahisha na cha kuhuzunisha amekua Kila kikifika kipindi cha usajili wamekua anaumia.

Ukumbusho kwamba anapokea pauni milioni 4.5 kwa mwaka kutoka kwa Manchester United bila kufanya lolote.

SIMBA QUEENS WAPEWA KAMSELELEKO LIGI YA MABINGWA AFRIKA WANAWAKE…CAF YAWAPA UHAKIKA…WAFELI WENYEWE TU… KUELEKEA MECHI YAO YA CAF KESHO…HAWA GEITA GOLD NAO HAWAKO KINYONGE AISEE….WAWATISHA WASUDAN…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply