Azam FC

KISA TABIA ‘ZA KIHUNI’ KWENYE MCHEZO DHIDI YA YANGA…AZAM WAMKALIA KITAKO BAJANA…KOCHA MZUNGU ‘AMMAINDI’..

admin September 10, 2022 8:29 am


Kocha wa makipa wa Azam FC, Dani Cadena amesema atakaachini na kuzungumza na kiungo, Sospeter Bajana baada ya kuonyesha kitendo cha utovu wa nidhamu katika mchezo wa juzi wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ulioisha kwa kufungana mabao 2-2.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa,  Bajana alitolewa ilinafasi yake kuchukuliwa na Cleophance Mkandala  jambo ambalo nyota huyo alionyweshwa kutokubaliana na mabadiliko hayo na kutoka moja kwa moja kwenda vyumbani.

Akizungumza jijini Dar es Salaam  baada ya mechi hiyo, Cadena alisema hakufurahishwa na kitendo alichio fanya Bajana kwani kimeonyesha taswira mbaya kitu ambacho atakaa naye ili kuzungumza ni kitu gani ambacho kilimpelekea  kufanya maamuzi yale.

“Nadhani alitamani kuendelea na mchezo kwa sababu kabla ya hapo alicheza vizuri na hata ukiangalia vizuri tayari inaonyesha wazi tempa ilishampanda ndio maana ikatokea vile japo siwezi kuzungumzia kwa sababu nitaongea naye,”

“Kwa liwango chake kiujumla amecheza vizuri japo nimefurahishwa na wachezaji wote kwa jinsi walipambana kuanzia mwanzo,  hii ndio mentality (mawazo) amabayo tunaijenga kwao ya kuhakikisha viwango vyao vinazidi kuimkarika.”

Cadena ndiye  aliye simamia timu hiyo kwenye mchezo huo baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi hicho, Abdihamid Moallin kupangiwa majukumu mengine huku Mfaransa, Denis Lavagne aliyetua juzi kwa ajili ya kuchukua mikoba hiyo akiwa jukwaani.

HII HAPA SIRI YA YANGA  KUEPUKA VIPIGO LIGI KUU KWA ZAIDI YA DAKIKA 3,600….NABI KAANIA YOTE YA NYUMA YA PAZIA… SIMBA QUEENS WAPEWA KAMSELELEKO LIGI YA MABINGWA AFRIKA WANAWAKE…CAF YAWAPA UHAKIKA…WAFELI WENYEWE TU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply