Habari za michezo

SIMBA WAIFANYIA UMAFIA NYASA BIG BULLETS …CHAMA AWAVURUGA WAMALAWI…WAPAGAWA NCHI NZIMA…

admin September 10, 2022 4:09 pm


Wawakilishi wa Tanzania katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC wameanza vyema kampeni ya kusaka kufuzu kwa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi ugenini nchini Malawi.

Simba wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi, magoli yaliyowekwa wavuni na Mshambuliaji Moses Phiri kipindi cha kwanza na John Bocco mwishoni mwa kipindi cha pili.

Gumzo kubwa katika mchezo wa Simba leo ni ufundi wa Kiungo wake raia wa Zambia Clatous Chotta Chama ambae ameonesha kandanda safi lililowapoteza Wamalawi.

Ushindi wa Simba ni hatua nzuri kwa Kocha mpya ndani ya Kikosi hicho Juma Mgunda ambae anasiamama kama kocha Mkuu katika kikosi hicho.

Simba watarudiana na Nyasa Big Bullets katika mchezo wa mkondo wa Pili utakaopigwa Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

MZIMU WA MOSIMANE WAENDELEA KUISUMBUA AL AHLY…WAINGIA GHARAMA KUBWA KUMPA KAZI “M’BAYA WA CHELSEA”… WASUDAN WAPARAMIA ‘MTUMBWI WA VIBWENGO’ KWA MKAPA…MAYELE ‘AWAPAPATUA TATU NA TUMBO’ JUU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply