Habari za michezo

WASUDAN WAPARAMIA ‘MTUMBWI WA VIBWENGO’ KWA MKAPA…MAYELE ‘AWAPAPATUA TATU NA TUMBO’ JUU…

admin September 10, 2022 4:15 pm


Kikosi cha Zalan FC wamekubali kichapo cha magoli 4-0 kutoka kwa wawakilishi wa Tanzania Yanga, mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar.

Mchezo huo wa hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika umewashuhudia Yanga wakitawala sehemu kubwa ya mchezo.

Alikuwa ni Fiston Mayele aliewapa uongozi Yanga sekunde chache tangu kuanza kwa kipindi cha pili kabla ya Feisal Salum kupachika bao la pili 55′ akimaliza kazi safi ya Fiston Mayele.

Dakika za 85 na 87 Mayele alirudi tena kambani na kupachika mabao 2 na kuhitimisha Hat-trick.

Yanga watarudiana na Zalan wikiendi ijayo mchezo wa mkondo wa pili kumpata mshindi wa jumla atakaekwenda hatua inayofuata.

SIMBA WAIFANYIA UMAFIA NYASA BIG BULLETS …CHAMA AWAVURUGA WAMALAWI…WAPAGAWA NCHI NZIMA… SAKATA LA MWAKINYO KUPIGWA UINGEREZA…MANDONGA NAYE KAONA ISIWE TABU…AIBUKA NA KUMSHUKIA KWA MANENO HAYA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply