Habari za michezo

BAADA YA KUWAZIBUA WAMALAWI JANA…UTAMU WA SIMBA WAMNOGEA MGUNDA…ATOA KAULI HII YA KIBABE…

admin September 11, 2022 5:51 pm


Haijaisha hadi iishe. Ni kauli ya Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda akielezea matokeo ya ushindi walioupata dhidi ya Nyasa Big Bullet katika mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika mkondo wa kwanza hatua ya awali, huku akimtaja Moses Phiri kuwa amekuja kufunga.

Simba imeibuka na ushindi wa 2-0 ikicheza ugenini katika uwanja wa Bingu uliopo Jiji la Lilongwe nchini Malawi na sasa itawasubiri wapinzani hao Jijini Dar es Salaam katika mchezo wa marudiano.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Mgunda amesema hawawezi kuwadharau wapinzani au kubweteka kwa matokeo hayo isipokuwa wanaenda kujipanga upya kuhakikisha wanaendeleza ushindi.

Amesema bado kazi haijaisha, huku akifichua siri kuwa ushindi wao umetokana na ushirikiano alioupata kwa wasaidizi wake akiwmao Seleman Matola.

“Haijaisha hadi iishe, siri ya ushindi huu ni ushirikiano kwa benchi la ufundi, Matola amenisaidia sana kunipa mwelekeo, kazi haijaisha tunasubiri mechi ijayo ili tufanye vizuri tena” amesema Mgunda.

Kuhusu Kasi ya Straika wake, Phiri Mgunda amesema Nyota huyo amesajiliwa kuja kufanya kazi na hiki anachofanya ni kutimiza wajibu wake.

“Kazi yake ni kufunga ndicho kimemleta Simba, hiki anachokifanya ndio jukumu lake” amesema Kocha huyo.

Kwa upande wake Kocha wa Nyassa Big Bullet Karisto Pasuwa, amesema kwa sasa wanaenda kujipanga na mechi ijayo huku akibainisha kuwa anaenda kukaa na vijana wake ili kutorudia makosa katika mechi ijayo.

“Vijana walipambana lakini umakini ulipungua katika kufunga mabao, wapinzani walipata nafasi hizo wakazitumia tunaenda kukaa upya kuona mechi ya marudio ugenini tufanya vizuri” amesema Pasuwa.

BAADA YA KUSEMWA SANA…HATIMAYE MWAKINYO AFUNGUKA A-Z KUHUSU BEGI LAKE…ADAI AMELIPATA… KOCHA MPYA AZAM AANZA KAZI NA GIA KUBWA…ATAMBA KUBEBA MAKOMBE MAKUBWA AFRIKA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply