Habari za michezo

DUH….KWA JAMBO HILI LA NABI …SASA NI ZAIDI YA SIFA…WASUDANI WAJIANDAE KWA KIPIGO KINGINE CHA ‘PAKA MWIZI’…

admin September 12, 2022 3:02 am


NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema bado kazi ipo kwenye mchezo wao ujao wa kimataifa dhidi ya Zalan FC.

Jana, Septemba 10, ubao wa Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ulisoma Zalan 0-4 Yanga huku wafungaji wakiwa ni Fiston Mayele aliyetupia mabao matatu na mzawa Feisal Salum aliyefunga bao moja.

Ushindi huo ulipatikana kipindi cha pili baada ya dakika 45 za mwanzo kila timu kukwama kumtungua mpinzani wake.

Nabi amesema:”Walishindwa kupata mabao ya mapema lakini tumetengeneza nafasi nyingi hiyo ilikuwa imetufanya tushindwe kuongeza hali ya kujiamini lakini kipindi cha pili tumeweza kupiga hatua kubwa.

“Mabadiliko yote ilikuwa ni kipindi cha pili unaona tulipopata bao la kuongoza iliongeza hali ya kujiamini hivyo bado tunazidi kuwa karibu na kutoka kwenye hatua hii kuelekea hatua inayofuata,” amesema.

Wikiendi ijayo timu hizo zinatarajia kurejeana Uwanja wa Mkapa ambapo ni Yanga atakuwa mwenyeji kwenye mchezo ujao.

Mshindi wa jumla atakwenda kukutana na mshindi kati ya Saint George ya Ethiopia ama Al Hilal ya Sudan kwenye hatua ya kwanza kimataifa.

PAMOJA NA SIMBA KUPATA USHINDI UGENINI…KUMBE JUMA MGUNDA ALIFANYA KAZI HII YA ZIADA KWENYE BENCHI… PAMOJA NA UWEPO WA WABRAZILI …MAMBO YAWA MAGUMU KWA KAGERE NA SINGIDA YAKE ….ISHU NZIMA IKO HIVI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply