Home Habari za michezo ACHANA NA SAKATA LA KISINDA ‘KUBANIWA KUCHEZA’…HAYA HAPA MAAJABU MENGINE YALIYOBAMBA KWENYE...

ACHANA NA SAKATA LA KISINDA ‘KUBANIWA KUCHEZA’…HAYA HAPA MAAJABU MENGINE YALIYOBAMBA KWENYE USAJILI BONGO…


JAPOKUWA ishu ya mjini kwa sasa ni usajili wa winga wa Yanga, aliyechukuliwa kwa mkopo kutoka RS Berkane ambako Wanajangwani hao walimuuza baada ya kumaliza msimu wa 2020/21, akiwa kwenye kiwango cha juu.

Baada ya usajili wake kumetokea sintofahamu kati ya Yanga na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mchezaji huyo kuonekana kama itakuwa ngumu kucheza Ligi Kuu Bara.

Ukiachana na hilo la Kisinda, yapo mambo mengi yaliyotokea wakati wa usajili wa msimu huu (2022/23) ambayo yalijadiliwa na wadau wa soka pamoja na kutamba kwenye mitandao ya kijamii.

HABIBU KYOMBO

Ukiachana na kwamba mashabiki wa Simba, hawakuonyesha kuchekelea usajili wa mshambuliaji Habibu Kyombo akitokea Mbeya Kwanza, mchezaji huyo alianza kusaini Singida Big Stars kisha Msimbazi (kudabo saini).

Kama SBS ingeamua kumkomalia Kyombo ingekuwa ishu nyingine ya kufanya makosa kusaini timu mbili ndani ya msimu mmoja, hilo nalo liligeuka gumzo, wakimshangaa mchezaji na Simba kuwania mchezaji wa aina yake na SBS.

SINGIDA BIG STARS

Japokuwa imepanda daraja kucheza kwa mara ya kwanza Ligi Kuu Bara, ilikuwa inashusha wachezaji wa kigeni wenye uwezo mkubwa, jambo ambalo liliwafanya wadau waiangalie timu hiyo kwa jicho la kiushindani zaidi.

Baadhi ya mapro waliopo SBS ni Pascal Wawa, Meddie Kagere,Bruno Gomes, Dario Federico, Joao Oliviera, Peterson Cruz, Carno Biemes, Miguel Escobar, Shafik Batambuze na Amisi Tambwe.

KISINDA VS TFF

Baada ya Yanga kumrejesha kwa mkopo aliyekuwa winga wao, Tuisila Kisinda ambaye ilimuuza RS Berkane ya Morocco mashabiki wake walipata furaha ya moyo, lakini ghafla wakajikuta wanachefukwa baada ya kusikia hatacheza Ligi Kuu.

TFF ilitoa taarifa Septemba 5, iliyokuwa ikielezea kanuni ya 62 (1) ya Ligi Kuu toleo la 2022 inayoeleza klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi 12, hivyo klabu kutaka ua kujaribu kusajili zaidi idadi hiyo ni kwenda kinyume na kanuni.

Wakati upande wa Yanga ulisema Kisinda alisajiliwa kwa wakati na wakaomba akatwe Lazarous Kambole aliyekuwa anasumbuliwa na majeraha, jambo ambalo lilileta sintofahamu kwa upande wa mashabiki na baadhi ya wadau wa soka nchini.

SOMA NA HII  MAYELE "NILIKUWA NAWATAMANI SANA RIVERS...WALITUTOA MAPEMA WAKAONGEA SANA

UTAMBULISHO WA WACHEZAJI

Staili ya utambulisho wachezaji ulikuwa wa aina yake kwa timu mbalimbali za Ligi Kuu mfano Yanga ilivyomtambulisha usiku wa manane Aziz Ki kutoka  Asec Mimosas na walianza kuweka ishara ya kufuri, iliyofanya mashabiki wasubiri hadi muda huo, kujua kinachojiri.

Ukiachana na Yanga, Simba ilikuwa na staili ya aina yake, ilikuwa inaandika jumbe kwenye mtandao wake wa kijamii (Instagram), kuwapa mashabiki taarifa muda na wanafanya jambo lao, walitumia maneno mazuri yayowapa hamu ya kusubiri muda wa tukio.

KAMBOLE KUKATWA

Jina la aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Lazarous Kambole aliyesajiliwa msimu huu, akitokea Kaizer Chief ya nchini Afrika Kusini, lilikatwa dakika za mwisho baada ya kusajiliwa Kisinda alikitokea RS Berkane ya Morocco.

Kurejea kwa Kisinda kuilazimu Yanga kumpunguza mchezaji mmoja wa kigeni, ikawa rahisi kuondolewa Kambole ambaye alikuwa anasumbuliwa na majeraha.

RUVU KUKOMAA NA WAZAWA

Kati ya timu 16 zinazocheza Ligi Kuu ni Ruvu pekee ndio haina mchezaji wa kigeni, huku mmoja wa kigogo wa juu akitoka sababu ya wachezaji wanakaa kambi za jeshi, ambayo haiwezi kuruhusu wageni kuzoea mazingira.

“Wachezaji wapo kambi ya jeshi ambayo inahitaji usiri mkubwa, hivyo hatuwezi kuwachukua wageni kuja kukaa nao huku ndio maana wamesajiliwa wazawa tu,” anasema Kigogo huyo.

Aina ya usajili wa msimu huu, umekuwa na mitazamo tofauti kwa wadau wa soka nchini, akianza kuelezea kocha Kenny Mwaisabula anayesema,

“Yanga, Simba, Azam FC, Singida Big Stars na Ihefu  natarajia zitaonyesha ushindani wa juu, kutokana na wachezaji wa kigeni waliopo kwenye timu zao.”

Kwa upande wa Beki wa zamani wa Simba, Frank Kasanga ‘Bwalya anasema, “Wageni wanaokuja wanapaswa wawe na ziada mbele ya wazawa, vinginevyo hakutakuwa na maana ya kuwasajili.”