Habari za michezo

RASMI…SUALA LA KISINDA KUZUIWA KUCHEZA BONGO…LAISHA KININJA….APEWA NAFASI YA KAMBOLE…WAGANDA WAOKOA JAHAZI…

admin September 15, 2022 4:29 pm

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepitisha usajili wa Twisila Kisinda kuichezea Yanga baada ya klabu hiyo kumuhamisha mchezaji wake wa kigeni Lazarous Kambole.

Awali Kamati hiyo ilizuia usajili wa Kisinda licha ya kuwa ulifanyika ndani ya dirisha la usajili kwa vile tayari Yanga ilikuwa na wachezaji 12 wa kigeni.

Licha ya changamoto hiyo, pia Kisinda aliombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ambayo tayari imepatikana.

Hivyo kwa kumuhamisha Kambole imepata nafasi ya kumsajili Kisinda kama ilivyokuwa imeshauriwa huko nyuma. Kwa mujibu wa Kanuni ya 62(1) ya Ligi Kuu Toleo la 2022, klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi 12.

Kambole amejiunga na timu ya Wakiso Giants inayocheza Ligi Kuu ya Uganda, na tayari TFF imetoa ITC.

ACHA KUNGOJA NGOJA AISEE…. KWA MTAJI WA TSH 100 UNATOBOA MAMILIONI…YOTE HAYA NI NDANI YA M-BET PEKEE… WAKATI YANGA WAKITAMBA KUWA NA BIGIRIMANA WAO….PACHA WAKE AIBUKIA KMC …KUANZA MAJAMBOZI NA IHEFU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply